Sunday, March 4, 2012

RAHA YA MAPENZI KUGOMBANA

MOJA ya hulka ya mwanadamu ni kutopenda amani na utulivu uliovuka mipaka. Hulka hii mwanadamu huianza tokea akiwa mtoto ndiyo maana unaweza kuona mtoto anahangaika mgongoni huku akiwa yuko kwenye mebeleko ya mama yake.

Si kwamba mtoto anahangaika kwa vile ana hofu ya kuanguka kutoka kwenye mgongo wa aliyembebea, la hasha, bali huwa amechoka na amani iliyopitiliza.

Akiwa mgongoni pale anakuwa yuko salama, ana kinga kamili kutoka kwa amtu aliyembeba, lakini bado hakubali atanyoosha mikono, atatoa miguu na kujirusha kama vile hafurahii kitendo cha kubebwa.

Mtoto anapokuwa katika mazingira haya sio kwamba hafurahii kubebwa wala si kuwa anatimiza ule msemo usemao "abebwaye hujikaza", hapana, bali hufanya hivyo katika kudhihirisha tu ile hulka ya mwanadamu kuwa huchoshwa hata na amani.

Ziko hata nchi ambazo huchokonoa hiki na kile na hatimaye kusababisha machafuko wakati kulikuwa na amani ya kutosha na kulikuwa hakuna hoja ya msingi ya kuwepo madai yoyote yale.

Hata kwenye uwanja wa mapenzi hali haiko tofauti. Ndiyo maana unaweza ukawaona watu wanaachana huku watu wengine wakishangaa kwa vile walikuwa wanawaona wana mapenzi mazito.

Hali hiyo inatokana na watu hao kuchoshwa na amani, kwa hiyo wanatafuta kila njia ili uwepo mgongano kati yao.

Bendi maarufu ya muziki wa dansi ya DDC Mlimani Park inayopiga mtindo wa Sikinde iliwahi kutoa wimbo mmoja ambao ulikuwa unazungumza juu ya wanandoa wanapogombana.

Katika wimbo huo inaelezwa kuwa mwanaume anakuwa mkorofi na anapokosana na mkewe na kurudi kwao anakwenda kutafuta suluhu.

Sikinde wanaeleza kwamba mwanaume huyo ambaye walimpa jina la "Chuma ulete" akiambiwa aangukie anatoa fedha nyingi kuliko mahari aliyotoa.

Ni ukweli usiobishika kwamba wako watu wa namna hii ambao wakigombana na wapenzi wao hulazimishwa kuangukia. Wako wanaotoa fedha, nguo, ng'ombe, mbuzi na vinywaji.

Hawa akina chuma ulete huwezi kuwalaumu hata kidogo kwani ndiyo hulka ya mwanadamu au ndio msingi wa maisha kuwa hakuwezi kuwa na utulivu na amani kupita kiasi.

Ndiyo maana hata maji kwenye mtungi hubumburika bila hata ya kuguswa na mtu au vyombo kwenye kabati hugongana bila ya kuwepo kwa mkono wa mtu.

Pamoja na kwamba ni vigumu kuwa na mapenzi yasiyoingiwa na migogoro hata kidogo; vinginevyo labda muwe munadanganyana kama wacheza sinema hivi, ni vizuri kujaribu kuipunguza kwa kadri inavyowezekana.

Lakini jambo la msingi zaidi inapotokea mgongano kati ya wapenzi ni kuhakikisha kwamba msiwe miamba wote wawili. Kila mmoja asijifanye kifaru na kutaka kuoneshana umwamba na mwenzake, hapo hamutafanikiwa na mapenzi yenu yanaweza kukatika huku munapendana.

Unapotokea ugomvi baina ya wapenzi si kwamba hawapendani tena au kuna mmoja kapata mwingine au anamchukia mwenzake, la hasha ni hali ileile tu ya kuwepo mikwaruzano ili maisha yawepo.

Kwa hiyo kinachotakiwa kutokea iwapo mgongano unazuka baina ya wawili wapendanao ni kwa mmoja kuwahi kuomba radhi na mwingine kuikubali hiyo rahi aliyoombwa bila ya kuweka masharti yoyote ya

10 WAYS TO THINK YOURSELF RICH
  1. Plan how to archieve it
  2. Nurture confidence
  3. Enjoy your work/ Business
  4. Become a risk- taker
  5. Start at the bottom
  6. Have respect for money
  7. Be open- minded
  8. Prepare to work hard
  9. Never ever give up!!!!!!!!!!!!!!

advice to all  friends.

drummer with fetyyy